JE, BIBLIA INASEMAJE LEO? - Masomo,Tafakari na Mwangaza wa Siku Leo Tarehe 05 June 2024
Mawaridi Media Mawaridi Media
11.8K subscribers
84 views
0

 Published On Jun 4, 2024

Masomo ya Misa 05/06/2024

Somo la Kwanza
2Tim. 1:1-3, 6-12
Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa ajili ya ahadi ya uzima ulio katika Kristo Yesu; kwa Timotheo, mwanangu mpendwa. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.
Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana.
Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele, na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili; ambayo kwa ajili ya hiyo naliwekwa niwe mhubiri na mtume na mwalimu.
Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.

NENO LA BWANA, TUMSHUKURU MUNGU.

Wimbo wa Katikati
Zab. 123:1-2
Nimekuinulia macho yangu,
Wewe uketiye mbinguni.
Kama vile macho ya watumishi
Kwa mkono wa bwana zao.
(K) Nimekuinulia macho yangu, ee Bwana.

Kama macho ya mjakazi
Kwa mkono wa bibi yake;
Hivyo macho yetu humwelekea Bwana, Mungu wetu.
Hata atakapoturehemu.
(K) Nimekuinulia macho yangu, ee Bwana.

Shangilio
Lk. 8:15
Aleluya, aleluya.
Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno la Mungu, na kulishika.
Aleluya.

Somo la Injili
Mk. 12:18-27
Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, walimwendea Yesu, wakamwuliza na kusema, Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mkewe wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mkewe akampatie ndugu yake mzao. Basi kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao. Wa pili naye akamtwaa akafa, wala yeye hakuacha mzao. Na wa tatu kadhalika; hata na wote saba, wasiache mzao. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. Basi, katika kiyama atakuwa mke wa yupi katika hao? Maana wote saba walikuwa naye.

Yesu akajibu, akawaambia, Je! hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu? Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni. Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Sura ya Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahi- mu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana.

NENO LA BWANA, SIFA KWAKO EE KRISTO.

Kwa Masomo ya Misa za kila siku, Sala mbalimbali na historia za maisha ya Watakatifu SUBSCRIBE KWENYE YOUTUBE CHANNEL HII ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA ZOTE KWA WAKATI.

TAFAKARI NA MWANGAZA WA SIKU.
"Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu."
Hayo ni maneno yaliyonenwa na mtume Paulo Kwa mwanafunzi wake Timetheo ambao walikuwa wakiubiri na KUINJIRISHA pamoja.
Kama tunavyojua Hadi mtu akutamkie maneno mema na yabaraka hivyo basi lazima upendo mkubwa uwe kati yenu.
Ivyo basi Kwa siku hii ya Leo tujiulize sisi wenyewe je, tumeacha ALAMA gani njema ya kukufanya ukumbukwe katika familia yako, Kwa wazazi wako, Kwa watoto wako, Kwa walimu wako, na kazini kwako bila kusahau kanisani kwako??
Hivyo basi katika siku hii ya Leo tunafundishwa tuweze kuwa watu wa kufanya mema ili tuweze kuacha ALAMA njema katika sehemu zetu.
"Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi."
Basi tuwe na Imani ya kwamba tunaweza.

Na katika SOMO LA INJILI tunaona masadukayo wakimuuliza habari za Kiyama au mwisho wa ulimwengu Bwana wetu Yesu Kristu na Cha kupata kuelewa katika SOMO hilo ni kuwa "Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno la Mungu, na kulishika." Lakini pia kuliishi kwani neno la Bwana nila adili na linataka utayari mkubwa wa kuweza kulitafakari.

TUMSIFU YESU KRISTU, MILELE NA MILELE AMINA.

NAKUTAKIA SIKU NJEMA NA YENYE BARAKA TELE MUNGU AKUONGOZE KATIKA KILA JAMBO ULIFANYALO NA UWEZE KUFANIKIWA.
NAOMBA USISAHAU KUGUSA ALAMA YA SUBSCRIBE HAPO CHINI ILI KUWEZA KUPATA MASOMO YA KILA SIKU NA TAFAKARI ZA KILA SIKU KWA WAKATI.

From #mawaridimedia

show more

Share/Embed