MASOMO, TAFAKARI NA MWANGAZA WA DOMINIKA YA SHEREHE YA MWILI NA DAMU TAKATIFU YA YESU Trh 02.06.2024
Mawaridi Media Mawaridi Media
11.8K subscribers
109 views
0

 Published On Jun 1, 2024

#catholic #mawaridimedia #dominika #misatakatifu #masomoyamisazakilasiku #dailymassreadingreflection


TAFAKARI, MWANGAZA NA MASOMO

Masomo ya Misa 02/06/2024

Somo la Kwanza
Kut. 24 : 3-8
Musa alienda akawaambia watu maneno yote ya Bwana, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena Bwana tutayatenda. Basi Musa akayaandika maneno yote ya Bwana, akaondoka asubuhi na mapema; akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli, akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia Bwana sadaka za amani za ng’ombe. Musa akatwaa nusu ya ile damu, akatia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainvunyiza juu ya madhabahu. Kisha akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii. Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote.
NENO LA BWANA, TUMSHUKURU MUNGU.

Wimbo wa Katikati
Zab. 116:12-13, 15-18
Nimrudishie Bwana nini
Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Nitakipokea kikombe cha wokovu;
Na kulitangaza jina la Bwana.
(K) Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la Bwana.

Ina thamani machoni pa Bwana
Mauti ya wacha Mungu wake.
Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako,
Umevifungua vifungo vyangu.
(K) Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la Bwana.

Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;
Na kulitangaza jina la Bwana;
Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana,
Naam mahali ya watu wake wote.
(K) Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la Bwana.

Somo la Pili
Ebr. 9:11-15
Kristo aliisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?
Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.
NENO LA BWANA, TUMSHUKURU MUNGU.

Shangilio
Yn. 6 :51
Aleluya, Aleluya,
Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; asema Bwana; mtu akila chakula hiki, ataishi milele.
Aleluya.

Somo la Injili
Mk. 14 :12-16, 22-26
Siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile pasaka? Akatuma wawili katika wanafunzi wake, akawaambia, Nendeni zenu mjini; atakutana nanyi mwanamume amechukua mtungi wa maji; mfuateni; na po pote atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu asema, Ki wapi chumba changu cha wageni, niile pasaka humo, pamoja na wanafunzi wangu? naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandikwa tayari; humo tuandalieni. Wanafunzi wakatoka, wakaenda mjini, wakaona kama alivyowambia. wakaiandaa pasaka.

Nao walipokuwa wakila, alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa akisema, Twaeni; huu ndio mwili wangu. Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote. Akawaambia, Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu. Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa Mizeituni.

NENO LA BWANA, SIFA KWAKO EE KRISTO.

Kwa Masomo ya Misa za kila siku, Sala mbalimbali na historia za maisha ya Watakatifu
USISAHAHU KUGUSA ALAMA YA SUBSCRIBE HAPO CHINI

TAFAKARI NA MWANGAZA WA SIKU

Dominika hii ya Leo tunakumbuka na kusherekea MWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTU aliye mchungaji mwema.

Katika SOMO la kwanza tunaona na kukumbushwa ni Kwa jinsi gani katika agano la kale kabla ya ujio wa YESU KRISTU walivyokuwa wakitoa sadaka Kwa ajili ya Kwa ajili ya kuomba msamaha wa Dhambi zao na kuomba utakaso wa Dhambi zao Kwa njia ya kuchinja wanyama na kutumia DAMU yao kama ishara ya kuomba msamaha
Rejea;
"akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia Bwana sadaka za amani za ng’ombe. Musa akatwaa nusu ya ile damu, akatia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainvunyiza juu ya madhabahu. Kisha akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii. Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi"


Lakini,
Katika SOMO la pili tunapata kuona ujio wa thamani sana.........
NAOMBA USISAHAU KUGUSA ALAMA YA SUBSCRIBE HAPO CHINI

show more

Share/Embed