Historia ya maisha ya watakatifu MASHAIDI WA UGANDA WAFIA DINI (MT. KALORI LWANGA NA WENZAKE)
Mawaridi Media Mawaridi Media
11.9K subscribers
68 views
0

 Published On Jun 4, 2024

MAISHA YA WATAKATIFU*

MT. KAROLI LWANGA NA WENZAKE

( 3 JUNI )

Wafiadini hawa 22 Wote ni Waafrika. Walipata taji la mbingu wakati wa Dhulumu ya Mwanga, Mfalme wa Uganda, kati ya miaka 1885 - 1887. Alipokuwa kijana, Mwanga alipendelea Sana kusikia mafundisho ya mapadre, alianza kuyaacha mambo yote ya kipagani, akawashauri watu wake wote waende kwa mapadre kufundishwa dini ya Yesu Kristu. Alichagua wakristu wengi akawapa kazi Bora zilizokuwa chini ya uwezo wake.

Wajumbe na raia wapagani walipoona kuwa mfalme wao
anakataa mambo yao ya kipagani, walipatana kwa faragha ili wa-mwue. Lakini siri yao ikajulikana kwa wakristu watatu waliokuwa watumishi wake. Mwanga aliwaita Katikiro (ndiyo Waziri Mkuu) wengine waliofanya shauri la kumwua, Lakini walipotubu kosa lao aliwasamehe.

Toka siku hiyo Katikiro, wa-zee na wafumu walikula njama Kuwaua wakristu. Kila siku wali-kwenda kwa mfalme Mwanga kuwashtaki kwa kumdanganya na kumwogofya. Kisha Mwanga ali-anza kudanganywa na mali na furaha mbaya za dunia; aliwashurutisha baadhi ya wakristu watende naye mabaya, lakini walikataa kishujaa kutenda hayo.
Hapo Mwanga aliwakasirikia, akataka kuwaua.

MATIASI MULUMBA alikuwa jumbe na kiongozi wa wazee washauri. Baba yake alipokuwa mzee alimwambia:
"Watakuja watu weupe na wataleta dini mpya. Utakapowaona uwapokee vizuri na uwasadiki".

Waarabu walipofika Uganda Mulumba aliwafuata. Lakini baada ya miaka michache wamisionari Waprotestanti walikuja huko Uganda. Mulumba aliyasikia mafundisho yao, akaya-Sadiki. Alipokuwa karibu ya kubatizwa, walikuja wamisionari Wakatoliki. Alipoyasikia mafundisho yao mara mbili, roho yake ikapata nuru, akajisikia ndani yake furaha kuu ambayo alikuwa hajaiona bado katika dini nyingine. Toka siku ile alifuata vema mafundisho ya Mapadre na tarehe 28 Mei 1882 alibatizwa pamoja na mkewe. Baada ya kubatizwa aliwa-fundisha watoto wake ili nao wawe wakristu. Alipendwa sana na watu wengine. Alijenga nyumba ya kulala kwa ajili ya watu wa mbali, ili wapate kuja kwenye mafundisho, na mara kwa mara aliwapa chakula.
Alipokamatwa na wauaji aliungama kwa uhodari dini yake. Alikatwa mikono, miguu, nyama ya mgongo akisema: "Ee Mungu wangu, Mungu wangu". Shahidi huyo alikufa 28 Mei 1886. Mungu aliwazuia wanyama porini na ndege wasiguse maiti ya mtumishi wake mwaminifu. Hivyo baada ya siku chache mapadre walikuja kuuchukua mwili wake wakauzika.

KAROLI LWANGA alikuwa kijana hodari, na wakati huo akiwa na umri wa miaka ishirini. Mfalme alimpenda kwa sababu alimwona ni mzuri, hodari, na pia alikuwa na tabia njema. Alimfanya msimamizi wa vijana mia tatu. Karoli aliwa-tangulia vijana wengine kusikiliza mafundisho ya mapadre, na vijana wengine walimfuata wakabatizwa. Mwanga aliposhikwa na tamaa mbaya za mwili alitaka kuwashawishi wale vijana kumridhia katika tamaa zake chafu. Karoli aliwasaidia vijana kujificha ili wapate kukaa na moyo safi. Aliwasaidia pia walipo kamatwa, hata aliwabatiza gerezani vijana wanne waliokuwa bado wakatekumeni. Siku moja asubuhi, kwa amri ya Mwanga, Karoli aliwa-kusanya vijana wote. Hapo Mwanga aliwaambia: "Kati yenu wale ambao hawataki kusali na kufuata dini ya kikristu wakae hapa karibu nami, na wale wanaotaka kusali na kufuata dini ya kikristu waende mbali kule ukutani." Baada ya Mwanga kusema hayo, Karoli Lwanga na kundi la Wakristu wote pamoja walienda kukaa ukutani. Waliungama kwa neno moja kwamba wao ni wakristu; tena hawataki kukana dini.

Kundi hilo lilikuwa na vijana 14 ndio: KAROLI
LWANGA, KIZITO, MBAGA TUZINDE, BRUNO SERUNKUMA YAKOBO BUZABALIAWO, AMBROSI KIBUKA, MUGAGA, GYAVIRA, ACHILE KIWANUKA, ADOLFO LUDIGO, MUKASA, ANATOLI KIRIGWAJO, ATANASI BAZEKUKETA, na GONZAGA
GONZA, Walifungwa pamoja wakapelekwa kilimani Namu-gongo, ili wakachomwe moto. Ilikuwa tarehe 3 Juni 1886 wali-poteketezwa katika tanuru la moto, wakafa wafiadini. Walikuwapo wengine walioungama dini wakati wa dhulumu hiyo.

YOSEFU MUKASA aliwatangulia wote. Alikuwa na umri wa miaka 26, na alikuwa msimamizi wa nyumba za Mfalme zenye vijana 500. Alikatwa kichwa, kisha akachomwa moto.

ANDREA KAGWA alikuwa na umri wa miaka 30. Katikiro alimwonea kijicho sana kwa sababu aliwafundisha wenzake ili wabatizwe, na tena alisikia kuwa mfalme anataka kumfanya Andrea Kagwa kuwa jemadari wa askari wake. Andrea pia alikatwa kichwa.

DIONISI SEBUGWAO alipigwa mkuki na Mwanga mwenyewe kwa sababu alimfundisha mwenzake katekisimu. Alikuwa na umri wa miaka 16.

inaendelea....

From #mawaridimedia

show more

Share/Embed