JE, BIBLIA INATUFUNDISHA NINI LEO? JUMATATU TAREHE 03.JUNE.2024 - MASOMO NA TAFAKARI YA SIKU
Mawaridi Media Mawaridi Media
11.9K subscribers
107 views
0

 Published On Jun 1, 2024

#catholicmass #catholic #mawaridimedia #masomoyamisazakilasiku #dailymassreadingreflection


Masomo ya Misa 03/06/2024

Somo la Kwanza
2Pet 1:2-7
Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika sabauri yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na ktika upendano wa ndugu, upendo.

NENO LA BWANA, TUMSHUKURU MUNGU.

Wimbo wa Katikati
Zab 91:1-2, 14-16
Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
(K) Mungu wangu ninakutumaini.

Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
Kwa kuwa amekaza kunipenda
Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, kwakuwa amenijua jina langu.
Ataniita nami nitamwitikia.
(K) Mungu wangu ninakutumaini.

Nitakuwa pamoja naye taabuni,
Nitamwokoa na kumtukuza;
Kwa siku nyingi nitamshibisha,
Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
(K) Mungu wangu ninakutumaini.

Shangilio
Zab 130:5
Aleluya, aleluya.
Roho yangu inamngoja Bwana, na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.

Somo la Injili
Mk 12:1-12
Yesu alisema na Mafarisayo kwa mifano; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akazungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Hata kwa wakati wake akatuma, mtumwa kwa wale wakulima, ili apokee kwa wakulima katika matunda ya mizabibu. Wakamtwaa, wakampiga, wakamtoa nje, hana kitu. Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, na huyo wakamtia jeraha -za kichwa, wakamfanyia jeuri. Akamtuma mwingine, huyo wakamwua; na wengine wengi, hawa wakiwapiga na hawa wakiwaua. Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu. Wakamkamata, wakamwua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu. basi atafanyaje yule bwana wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine. Hata andiko hili hamjalisoma, Jiwe walilolikataa waashi, hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni. Neno hili limetoka kwa Bwana, nalo ni ajabu machoni petu? Nao wakatafuta kumkamata, wakaogopa mkutano; maana walitambua ya kwamba ule mfano amewanenea wao. Wakamwacha wakaenda zao.

NENO LA BWANA, SIFA KWAKO EE KRISTO.

Kwa Masomo ya Misa za kila siku, Sala mbalimbali na historia za maisha ya Watakatifu SUBSCRIBE KWENYE YOUTUBE CHANNEL HII.


TAFAKARI NA MWANGAZA WA SIKU.
Rejea;
Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika sabauri yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na ktika upendano wa ndugu, upendo.

✓IMANI
👇
✓WEMA
👇
✓MAARIFA
👇
✓KIASI
👇
✓SABURI
👇
✓UTAUWA
👇
✓UPENDANO WA NDUGU
👇
✓UPENDO

Ivyo basi katika siku ya Leo na daima katika maisha yetu ya tupasa kufuata mfululizo au mfuatano huo kama mwongozo wetu tukitaka kuwa wema na wanaopendeza mbele ya Mungu muumbaji wetu. Kwani ukifuatilia kweli na kuufuata kweli mfululizo huo utanikuta unatimiza amri za Mwenyezi Mungu na unamuruhusu Roho Mtakatifu aweze kukaa na kukuongoza wewe katika maisha yako ya Kila siku.

Na katika SOMO LA INJILI, tumeona Bwana wetu Yesu Kristo akiwa anaongea na Mafarisayo Kwa mifano ambayo kupitia mfano huo, inatufundisha kuwa Dunia hili ni sawa na shamba la mizabibu ambapo Mungu muumbaji ni mwenye shamba hili na katika shamba hili Kuna wafanyakazi au wakulima ambao ndo sisi wanadamu, hivyo basi sisi wanadamu tunaletewa NENO la uzima, mbegu ya uzima lakini sisi tunalikataa Kwa kuwakataa wale waliotumwa na Mungu ambao ni manabii wake wa hapo mwanzo hivyo basi anamua kumtuma wanaye wa pekee ili aje kwetu na yeye tunamkataa pia Kwa kumuua tukisema ya kuwa yeye ndiye hatakaye kuja kuurithi ufalme wa Mungu ivyo basi Mungu mwenyewe anatukasilikia na kuamua kuja kuiangamiza na kuiteketeza Dunia nzima na vyote vilivyomo ambao ndo utakuwa mwisho wa ulimwengu.
Hivyo basi nawasii wenzangu tumkimbilie na tumpokee Mungu Kwa roho na kweli ili aweze kukaa kwetu na kuwa mwenye huruma kwetu KUPITIA kutenda Yale yampendezayo.

TUMSIFU YESU KRISTU, MILELE NA MILELE AMINA.
NAKUTAKIA SIKU NJEMA NA TAFAKARI NJEMA KWA KUMFANYA MUNGU AWE MWONGOZO WAKO.


NAOMBA USISAHAU KUGUSA ALAMA YA SUBSCRIBE HAPO CHINI ILI KUWEZA KUSHIRIKI KUINJIRISHA NA KUFIKISHA NENO LA BWANA KWA WATU WOTE.

show more

Share/Embed