TAFAKARI YA MASOMO YA MISA LEO TAREHE 30/05/2024 // Daily Catholic mass readings and Reflection
Mawaridi Media Mawaridi Media
11.9K subscribers
104 views
0

 Published On May 29, 2024

MASOMO YA MISA 30/05/2024

Somo la Kwanza
1Pet 2:2-5, 9-12
Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili. Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.

NENO LA BWANA TUMSHUKURU MUNGU.

Wimbo wa Katikati
Zab 100:2-5
Mtumikieni Bwana kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba;
(K) Njoni mbele za Bwana kwa kuimba kwa furaha

Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
(K) Njoni mbele za Bwana kwa kuimba kwa furaha

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;
(K) Njoni mbele za Bwana kwa kuimba kwa furaha

Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi.
(K) Njoni mbele za Bwana kwa kuimba kwa furaha

Shangilio
Yn 8:12
Aleluya, Aleluya
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya

Somo la Injili
Mk 10: 46-52
Walifika Yeriko; Yesu alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia. Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu. Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu. Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita. Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu. Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.

NENO LA BWANA SIFA KWAKO EE KRISTO.









01:TAMAA

yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;





mmejengwa mwe nyumba ya Roho,










02:KUWA KIOO
Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.













03:IMANI
Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu

#mawaridimedia #masomoyamisa
#catholicmass #dailyreadings
#misa #dailymassreadingreflection

show more

Share/Embed