TAFAKARI NA MWANGAZA WA SIKU WA BIBLIA TAKATIFU - Masomo ya Misa ya Leo tarehe 01.06.2024
Mawaridi Media Mawaridi Media
11.8K subscribers
145 views
0

 Published On May 31, 2024

#catholic #mawaridimedia #catholicmass #masomoyamisazakilasiku


TAFAKARI NA MWANGAZA WA SIKU


Masomo ya Misa 01/06/2024

Somo la Kwanza
Yud. 17:20-25
Wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo,
Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu, jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele. Wahurumieni wengine walio na shaka, na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.
Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu; Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina.

NENO LA BWANA, TUMSHUKURU MUNGU.

Wimbo wa Katikati
Zab. 63:1-5
Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu,
Mwili wangu wakuonea shauku,
Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
(K) Nafsi yangu inakuonea kiu, Ee Bwana.

Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,
Nizione nguvu zako na utukufu wako.
Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai;
Midomo yangu itakusifu.
(K) Nafsi yangu inakuonea kiu, Ee Bwana.

Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;
Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono;
Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
(K) Nafsi yangu inakuonea kiu, Ee Bwana.

Somo la Injili
Mk. 11:27-33
Yesu na wanafunzi walifika Yerusalemu; alipokuwa akitembea hekaluni, walimwendea wakuu wa makuhani, na waandishi, na wazee, wakamwambia, Ni kwa mamlaka gani unatenda mambo haya? naye ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya? Yesu akawaambia, Nitawauliza neno moja, nanyi mnijibu, kisha nitawaambia ni kwa mamlaka gani nayatenda haya. Ubatizo wa Yohane ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Nijibuni.
Wakasemezana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema, Ulitoka mbinguni, atasema, Mbona, basi, hamkumwamini? Ila tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, -- waliogopa watu; maana watu wote walimwona Yohana kuwa nabii halisi. Wakamjibu Yesu, wakasema, Hatujui. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani nayatenda haya.

NENO LA BWANA, SIFA KWAKO EE KRISTO.

Kwa Masomo ya Misa za kila siku, Sala mbalimbali na historia za maisha ya Watakatifu NAOMBA USISAHAU KUGUSA ALAMA YA SUBSCRIBE HAPO CHINI



TAFAKARI YA SIKU
Leo ni jumamosi ya kwanza baada ya sikuu ya pentecoste ambapo Kadiri ya Kanisa katoliki Leo ni siku ya kuadhimisha MOYO SAFI WA BIKIRA MARIA ivyo basi katika siku hii ya Leo TUWEZE kumuomba Mwenyezi Mungu aweze kutujalia moyo safi kama wa mama yake Bikira Maria Kwa kuwa na UPENDO usio na kifani Kwa Mungu mwenyewe, wazazi wetu, ndugu zetu na marafiki zetu lakini pia kupitia UPENDO huo tuweze kuwa watu wa kutenda na kuyaishi Yale yanayo mpendeza Mwenyezi Mungu na kuukimbia uovu pamoja na Yale yasiyompendeza Mwenyezi Mungu yaani DHAMBI
Rejea:
"Wahurumieni wengine walio na shaka, na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu"
Ivyo basi tunawajibu nasi pia kuwaongoz wenzetu / ndugu zetu/ marafiki wetu katika Njia inayompendeza Mungu na ndo inamaana Kuna msemo unaosema "nitajie rafiki yako nikwambie tabia yako"
Kumbe nasi pia inatupasa kuwa marafiki wa kweli na wafaida mbele ya wenzetu Kwa kuwaongoza katika Njia iliyo njema.


Na katika SOMO LA INJILI tunamwona Yesu akitufundisha na kutwambia kama tunataka kitu chochote basi nasi ya tupasa kutoa kitu tulicho nacho,
Tukirejea msitari ulikuwa ulisema "wakuu wa makuhani, na waandishi, na wazee, wakamwambia, Ni kwa mamlaka gani unatenda mambo haya? naye ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya? Yesu akawaambia, Nitawauliza neno moja, nanyi mnijibu, kisha nitawaambia ni kwa mamlaka gani nayatenda haya. Ubatizo wa Yohane ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu?"
Hivyo basi kama unataka kitu chochote na wewe yakupasa uwe na ufahamu juu ya kitu hicho. Kwamfano; kama unataka kufanya vizuri sana katika biashara yako nawewe yakupasa uwe na juhudi juu ya biashara yako hiyo vivyoivyo Kwa wanafunzi soma kwanza uwe na kitu afadhari kichwani Kisha muombe Mungu akuongoze kutumia ufahamu na maarifa hayo kujibu mtihani wako na ndo inamaana aliwajibu akisema "Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani nayatenda haya"

TUMSIFU YESU KRISTU WAPENDWA....

NAOMBA USISAHAU KUGUSA ALAMA YA SUBSCRIBE ILI KUWEZA KUPATA MASOMO NA TAFAKARI ZA KILA SIKU.

show more

Share/Embed