SEHEMU ULIYOPO INAVYOWEZA KUHUSIKA KUPINGA MAFANIKIO YAKO - PASTOR SUNBELLA KYANDO
Reality of Christ Church Reality of Christ Church
76.9K subscribers
197,212 views
1.7K

 Published On Aug 28, 2021

Kuna wakati mtu unaomba sana,unafunga sana lakini bado mambo hayafunguki.Na hata ukienda kuombewa bado hakuna nguvu ya giza ambayo inakutwa ndani yako.
Kuna matatizo mengine chanzo sio wewe bali eneo unaloishi au unalofanya kazi.Kuna watu tangu wahamie nyumba fulani tu ndio uchumi umeshuka,ndoa zimeharibika,kibali kimeondolewa n.k

Ukisoma kitabu cha Mwanzo 28:10-16 utaona habari ya Yakobo,namna ambavyo baada ya kulala pale Luzu(ambapo baadae alipaita Betheli) aliota ndoto na akaona lango la mbinguni likiwa wazi na malaika wanapanda na kushuka.Alipoamka alijua kabisa na akasema kuwa pale ni lango la mbinguni wala hakujua.Katika eneo lile Mungu alisema nae juu ya habari za kumbariki na ahadi ambazo ameahidi juu yake.
Lakini ukisoma Mwanzo 12:7-8 inaelezea chanzo cha lango hilo kuwepo, Ibrahim alimtengenezea Bwana madhabahu mahali hapo akatoa na sadaka.Na baada ya hapo kutoka kwa Ibrahim hadi kwa Yakobo ni miaka mingi ilipita(maana Yakobo ni mjukuu wa Ibrahim) lakini ile madhabahu aliyoiinua Ibrahim ikatengeneza lango na bado ilikuwa inafanya kazi.
Unachotakiwa kujua ni kuwa,kama mtu anaweza kutengeneza madhabahu ya Mungu na nguvu ya hiyo madhabahu ikafanya kazi hata kwa vizazi vya mbele baada yake,vivyo hivyo katika upande wa giza.Eneo unalokaa au unalofanya kazi huko nyuma lina historia ambayo huijui ambayo kwa hiyo mambo yako yanaweza kufunguka au kufunga, inategemea na kilichofanyika hapo kama ni cha Mungu au ni cha shetani.


UNAWEZA WASILIANA NASI AU KUTUMA SADAKA YAKO KWA NAMBA HII : 0657 173 322
Unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii
Like our Facebook:   / therealityof.  .
Follow our Instagram:   / realityofch.  .
Subscribe our YouTube: https://www.youtube.com/channel/UC67L...
Also Subscribe Roc worshippers youtube channel:   / @rocworshipperz  

show more

Share/Embed