WANAUME WAMEKIMBIA WAMETUACHIA FAMILIA KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE, MVUTANO UJENZI WA SHULE MPYA
Millard Ayo Millard Ayo
5.22M subscribers
894 views
11

 Published On Jul 1, 2024

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mtandika Kilichopo kata ya Ruaha Mbuyuni Wilaya ya Kilolo wamelalamikia serikali kuelekeza kujengwa kwa shule mpya wakati Shule iliyopo ya msingi Kidika ina madarasa matatu pekee na haijamalizika.

Zaidi ya Shilingi Millioni 350 zimewekwa katika akaunti ya Shule ya msingi Kidika na kuelekeza kujengwa shule mpya.

Wakiongea katika Mkutano huo wa Kijiji baadhi ya wananchi wameonekana kushangazwa na Maamuzi ya kushindwa kumalizia shule iliyopo ambayo Ina Madarasa matatu iliyojengwa Kwa nguvu za wananchi.

Hata hivyo mwenyekiti wa Kijiji cha Mtandika Adam Makunga anasema Muongozo uliotoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo zinaelekeza pesa hizo kujengwa shule mpya. Hata hivyo mkutano huo ulielekeza maeneo mawili ambayo Shule Hiyo mpya inatakiwa Kujenga hivyo wanasubiri wataalam Ili kuweza kutazama mazingira kama ni Rafiki Kwa Ujenzi wa shule.

show more

Share/Embed