MAADHIMISHO YA SIKU YA UPANZI WA MITI YAFANYIKA ISIOLO
Waso TV Waso TV
4.97K subscribers
94 views
1

 Published On May 10, 2024

Ikiwa ni siku ya maadhimisho ya upanzi wa miti nchini , kaunti ya isiolo imefanyika hafla hiyo katika shule ya walemavu wa kusikia yaani school for the deaf ilioko eneo la chechelesi . hafla hiyo imeongozwa na kamishna wa gatuzi la isiolo Geoffrey Omoding.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, bwana omoding amesema kwamba kaunti ya isiolo kutapandwa miche elfu kumi , huku ikitarajiwa kufikia mwaka 2032 kupandwe miche elfu kumi na tano kote nchini .

Hata hivyo kamishna huyo ametoa wito kwa wakazi wa isiolo kuepuka kuvuka mito ambayo imefurika ili kuzuia maafa kutokea na kutoa agizo kwa walimu wakuu wa shule za msingi na wasimamizi wa shule kutathmini hali ya vyoo ambavyo vimeharibiwa na mafurika kabla shule kufunguliwa mnamo tarehe 13 wiki ijayo .

Hayo yakijiri , bwana Joseph Mbugua ambaye ni mhifadhi wa misitu kaunti ya isiolo yaani county forest conservator ,amesema kwamba kiwango cha misitu kaunti ya isiolo ni asilimia 5.6 na kiwango cha miti ni asilimia 6.7 lakini wakaazi na washikadau wakiweka juhudi za kupanda miti nyingi , viwango hivyo vitaongezeka .

Hafla hiyo ilihudhuriwa na maafisa wa misitu, wa polisi, maafisa wa mamlak ya Mto Ewaso Ng'iro yaani Ewaso Ng'iro north development Authority na wanfunzi wa chuo cha mafunzo ya matibabu isiolo , kmtc.

Join this channel to get access to perks:
   / @wasotv  

WASO TV - Informing and Entertaining

show more

Share/Embed