Wanafunzi wa Wilaya za Morogoro waelimishwa kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya
DCEA TV DCEA TV
531 subscribers
35 views
0

 Published On Sep 24, 2024

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imetoa elimu ya dawa za kulevya mkoani Morogoro hususan katika wilaya za Mahenge, Malinyi, na Mvomero kwa wanafunzi na walimu kutoka shule za sekondari za Kasita, Nawenge, Kwiro, Usangule, Don Bosco, na Mzumbe.


Utoaji wa elimu hiyo katika Mkoa wa Morogoro, ni moja ya mkakati wa kujenga uelewa juu ya tatizo la dawa za kulevya hasa ikizingatiwa kuwa, mkoa huo unakabiliwa na changamoto kubwa ya kilimo cha bangii hali inayohatarisha ustawi wa jamii hususani vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa.

Mamlaka imeweka mkazo kwa wanafunzi na walimu pia katika klabu za wanafunzi za kupambana na rushwa na dawa za kulevya kwa sababu kundi hili lina nafasi kubwa ya kufikisha ujumbe kwa hadhira juu ya madhara ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Aidha, katika kuhakikisha elimu sahihi inatolewa katika jamii hiyo, DCEA imetoa miongozo maalum kwa walimu na walezi wa klabu za Kupambana na Rushwa na Dawa za Kulevya katika shule hizo ili kuwasaidia kutoa elimu kuhusu kusudiwa kwa usahihi.

show more

Share/Embed