Musukuma: "Faini ya Bodaboda iwe Elfu 2 au Buku I Rais Samia Ametoa Milioni 500 Kila Jimbo"
CLOUDSMEDIA CLOUDSMEDIA
1.35M subscribers
164,754 views
687

 Published On Jun 14, 2021

"Nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya lakini pia kwa usikivu, sisi wabunge tumekuwa na mambo mengi na tumelalamika kwa muda mfupi na kwa muda mchache aliokaa madarakani ameanza kutekeleza, kila mbunge hapa amepata milioni 500 kwenye jimbo."

"Nilikuwa najiuliza wachumi wetu mko namna gani, inawezekanaje bodaboda inayobeba abiria wawili inakuwa na faini sawa na basi linalobeba abiria 65, mimi nashauri hata hiyo elfu 10 bado ni nyingi tungeweka hata elfu 2, lengo letu sio faini, lengo ni kuwawezesha watu watoke kwenye bodaboda wanunue magari, hakuna mtu anapenda kuendesha bodaboda miaka 5 anaumia kifua. Tumeanza vizuri kwenye elfu 10 lakini nashauri tufikirie kwenda kwenye elfu mbili au hata "buku" kwani kuna shida gani, nchi ina pesa nyingi"

#KutokaBungeni
#CloudsDigitalUpdates

show more

Share/Embed