Wataalamu mbalimbali kutoka Kisii wakutana kujadili na kuunga mkono mfumo wa Azimio la Umoja
KTN News Kenya KTN News Kenya
2.91M subscribers
12,367 views
66

 Published On Jan 25, 2022

Wataalamu mbalimbali kutoka kaunti ya Kisii wanakutana kujadili na kuunga mkono mfumo wa Azimio la Umoja katika kuunga mkono azma ya urais ya kiongozi wa ODM Raila Odinga. Kwenye mkutano uliofanyika katika kituo cha mafunzo ya kilimo huko Kisii, viongozi hao wametaka kuwe na uwiano miongoni mwa viongozi wa jamii ili kusukuma ajenda sawa katika ukanda wa nyanza nzima. Vyama vilivyowakilishwa kwenye mkutano huo kama ODM, Jubilee na KNC vimeapa kumuunga mkono Odinga kwenye uchaguzi mkuu. Uongozi wa kaunti ya Kisii ukiongozwa na gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae na Seneta Prof Sam Ongeri wamezitaka jamii zinazoishi maeneo hayo kuunga mkono ajenda ya Azimio la Umoja na kumpigia kura Raila Odinga.

show more

Share/Embed