MAGOLI Yote ya Simba Vs Al Masry 2-2
Global TV  Online Global TV Online
5.03M subscribers
126,321 views
180

 Published On Mar 7, 2018

MAGOLI Yote ya Simba Vs Al Masry 2-2

MCHEZO wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC na Al Masry ya Misri umemalizika kwa sare ya 2-2 usiku huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanamaanisha Simba SC wanahitaji kwenda kupigania ushindi wa ugenini siku 10 zijazo mjini Cairo, Misri ili kusonga mbele.
Mchezo huo ulisimama kwa takriban nusu saa kuanzia dakika ya 83 kufuatia umeme kukatika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam timu hizo zikiwa zimefungana mabao 2-2.
Refa Hando Helpus aliyesaidiwa na Zakjele Thusi na Athenkosi Ndongeni wote kutoka Afrika Kusini alilazimika kusimamisha mchezo huo baada ya umeme kukatika ghafla dakika ya 83, dakika 10 tu baada ya Simba kusawazisha bao la pili.
Wakati huo, tayari mvua kubwa ilikwishaanza kunyesha Uwanja wa Taifa na kusababisha baadhi ya mashabiki kuanza kuondoka kwa kuhofia usalama wao.
Katika mchezo huo uliokuwa wa ushindani mkali, Simba walitangulia kupata dakika ya tisa tu kupitia kwa Nahodha wake, mshambuliaji John Raphael Bocco aliyefunga kwa penalti baada ya mchezaji wa Al Masry, Mohamed Koffi kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Bao hilo halikudumu sana, kwani Ahmed Goma aliisawazishia Al Masry inayofundishwa na gwiji wa Misri, Hossam Hassan dakika ya 11 kwa shuti lililomshinda kipa Aishi Manula.

Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe    / uwazi  

FACEBOOK:   / globalpublis.  . TWITTER:   / globalhabari   Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe    / uwazi1  

kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…    / uwazi1      / uwazi1      / uwazi1   WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK:   / globalpublis.  . TWITTER:   / globalhabari   INSTAGRAM:   / globalpubli  .

show more

Share/Embed