WAZIRI WA AFYA AWASHA MOTO OCEAN ROAD
Mwananchi Digital Mwananchi Digital
1.02M subscribers
47,616 views
227

 Published On Jan 6, 2021

Dar es Salaam. Waziri wa Afya Dk Doroth Gwajima amepiga marufuku maofisa wa wizara kuingia mikataba ya aina yoyote inayohusisha kuagiza mashine za matibabu kwenye taasisi na badala yake jukumu hilo liachwe kwa taasisi husika.

Amesema wizara itakuwa na jukumu la kutafuta fedha na miradi lakini mikataba ya ununuzi wa mashine itaingiwa na taasisi husika ili kuwapa fursa ya kuchagua mashine inayowafaa na wanayoweza kuisimamia hasa inapohitaji matengenezo.

Agizo hilo amelitoa baada ya ziara yake katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) na kubaini uwepo wa mashine mbili zenye dosari, moja ikiwa haifanyi kazi kabisa huku nyingine ikiwa na mapungufu katika ufanyaji kazi wake.

Mojawapo ya mashine hizo ni ya X ray ya kisasa (digital Xray) ambayo licha ya kuwa na uwezo wa kufanya vipimo vingi kwa wakati na kutoa majibu ya uhakika imeelezwa kuwa na vikwazo katika uchukuaji wa picha kulingana na hali ya mgonjwa husika.

Nyingine ni mashine inayotumika kupima saratani ya matiti (mammography machine) ambayo iliharibika Novemba 30 mwaka jana ikiwa ni miezi miwili baada ya kufikishwa katika taasisi hiyo na kuanza kutumika.

Akiwa kwenye chumba cha Xray, Dk Gwajima alihoji ufanyaji kazi mashine hiyo huku akieleza kuwa tayari anazo taarifa za ndani ndipo alipoelezewa mapungufu yake.

show more

Share/Embed