Tanzania Bara 0-2 Kenya | Magoli na sherehe za ubingwa (Fainali Cecafa Women Cup - 25/11/2019)
Azam TV Azam TV
2.66M subscribers
29,408 views
0

 Published On Nov 25, 2019

Kenya wameibuka mabingwa wapya wa michuano ya CECAFA kwa wanawake mwaka 2019, wakiwapokonya tonge mdomoni, Tanzania Bara.

Ubingwa huo ni baada ya kushinda mabao 2-0 kwenye mechi ya fainali iliyochezwe leo jioni Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Jijini Dar es Salaam.

Jahazi la Tanzania Bara, limezama kwa magoli mawili yaliyofungwa na mshambuliaji hatari, Jentrix Shikangwa, katika dakika ya 71 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 88 kwa shuti kali.

Haya hapa magoli ya Kenya kwenye mechi hiyo ya fainali na jinsi Kenya walivyokabidhiwa kombe, wakiivua Ubingwa Kilimanjaro Queens, ambayo ilikuwa imetwaa mara mbili mfululizo.

show more

Share/Embed