SPIKA AMUONYA CAG - "Una Dharau Sana, Umetuita Dhaifu"
Global TV  Online Global TV Online
5.01M subscribers
195,487 views
621

 Published On Jan 7, 2019

SPIKA AMUONYA CAG - "Una Dharau Sana, Umetuita Dhaifu"

SPIKA wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, kuripoti mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka, Januari 21, 2019, na asipofika atapelekwa akiwa amefungwa pingu na polisi.

Ndugai amesema hayo leo Jumatatu Januari 7, 2019 wakati akizungumza na na waandishi wa habari mjini Dodoma na kumtaka Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee kuripoti mbele ya kamati hiyo Januari 22, kwa madai kuwa wawili hao kwa nyakati tofauti walisema Bunge ni dhaifu.

Alichosema CAG

Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Arnold Kayanda, alimuuliza CAG kuwa ofisi yake imekuwa ikijitahidi kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa ripoti zenye kuonyesha kuna ubadhirifu lakini baada ya hapo wananchi hawaoni kinachoendelea.

CAG alijibu: “Hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge. Kama tunatoa ripoti zinazoonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu ni udhaifu wa Bunge. Bunge linatakiwa kusimamia na kuhakikisha pale panapoonekana kuna matatizo basi hatua zinachukuliwa.

“Sisi kazi yetu ni kutoa ripoti. Na huu udhaifu nafikiri ni jambo lenye kusikitisha. Lakini ni jambo ambalo muda si mrefu huenda litarekebishika. Ni tatizo kubwa ambalo tunahisi Bunge linashindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa.”

Akiendelea kufafanua jibu lake, CAG Assad alisema: “Sitaki kuwa labda nasema hili kwa sababu linahusisha watu fulani, lakini ninachotaka kusema ni kuwa Bunge likifanya kazi yake vizuri, hata huu udhaifu unaoonekana utapungua.”

Mwaka 2018 lilipoibuka suala upotevu wa Sh trilioni 1.5 kwenye hesabu za serikali mwaka wa fedha 2016-2017, Assad aliulizwa kuhusu nini kifanyike, akataka Bunge liulizwe kwani ndilo lenye kutakiwa kuibana serikali kuhusu kutoonekana kwa fedha hizo.

Alichokisema Mdee

Baada ya kauli hiyo ya Profesa Assad, wiki iliyopita Halima Mdee alihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu alichokisema CAG na kukubaliana na hoja zake.

Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitte

www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho USIKUBALI KUPITWA NA HII, BONYEZA LINK https://www.youtube.com/watch/L4UGw.

show more

Share/Embed