HATIMAE ILE BANDARI YA 'WATER TAXI BOAT' RAMANI IMETOKA RASMI LEO, SMZ YATILIANA SAINI
KTV TZ ONLINE KTV TZ ONLINE
375K subscribers
12,434 views
0

 Published On Premiered Jan 9, 2024

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali
Mwinyi, amesema serikali ina kila sababu ya kufanya mabadiliko makubwa katika sekta ya baharini ili kuweka mazingira mazuri ya usafiri wa bahari kwa wananchi wa Zanzibar na wageni wanaoingia nchini .
 
Dk. Mwinyi alieleza hayo mara baada ya kushuhudia hafla ya utiaji saini
mkataba wa ujenzi bandari ya abiria Mpigaduri Maruhubi baina ya wizara
ya Mawasiliano na Uchukuzi chini ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Khadija
 CHINI YA na kampuni ya  Zanzibar for a Brighter Future ZF Devco Ikulu
Mjini Zanzibar.
 
Alisema serikali imeamua kujenga bandari ya mpiga duri kutokana na
bandari ya Malindi ya abiria kuzidiwa,kuleta msongamano mkubwa na hata usalama wake kuwa mdogo.
 
Aidha alisema mradi huo itakuwa mfano mkubwa wa ushirikiano wa sera
ya serikali na sekta binafsi ya PPP katika kufikia malengo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.
 
Alibainisha kuwa serikali haikuweza kuivunja bandari ya Malindi bali
imeamua kujenga eneo jengine la mpiga duri ambayo itahusisha maeneo
tofauti ikiwemo eneo la abiria la kisasa.
 
Dk. Mwinyi alibainisha kuwa mradi huo utakapokamilika ni ni fursa kubwa
ya biashara na wameamua kuingia makubaliano ili nchi iweze kufaidika
kiuchumi na kuondosha changamoto ya usafiri kwa wananchi wa Zanzibar
hasa kwa wasafiri wanaotoka kisiwani Pemba na Dar- es salam.
 
“Abiria waopita hapo ni kati ya 5000 mpaka 12,000 kwa siku hiyo ni fursa
kubwa ya biashara, wenzetu tumezungumza nao na tumeshirikiana na leo
tumeamua kwa pamoja kuingia mashirikiano ili kuweza kufaidika
kibiashara, kiuchumi na pia kutoa huduma bora kwa wananchi wetu,”
alibainisha.
 
Rais Mwinyi alibainisha kuwa  serikali imejipanga kuwa na usafiri wa aina
mbalimbali ikiwemo usafiri wa barabara kwa kuwa na mabasi ya gesi na
umeme ,treni na usafiri wa majini kwa kutumia water tax.
.....................................................................................................
Angalia Video Hii Mwanzo mwisho , Kisha Subscribe ili uendelee Kupata Habari Zote.

Follow Ktv Tz Online
Facebook | KTV TZ ONLINE
INSTAGRAM |@ktv_tz_online

Wasiliana nasi kupitia number
+255 717 619 834



Ktv Tz Online Journalists

cc: Sadia Rashid
cc: Sauti Byego

Camera Department"
Dadi Ali
Omar (OJ)
Nassor Shaibu
Abdallah Juma

Editors:
Juma Maulid
Dadi Ali




Video Zingine:
Angalia hapa - Diamond Platnumz Alivyolisha watoto yatima
- Ali Kiba akiwa Oman

   • ALICHOKIFANYA DIAMOND ZANZIBAR HAITOS...  
   • NI KWELI ALI KIBA AMNUNULIA NYUMBA OM...  

show more

Share/Embed