GWAJIMA ATAKA MAMLAKA YA RAIS YAFUNGWE KISHERIA | KUNA SIKU TUTAANGUKIA PUA
TBConline TBConline
413K subscribers
49,656 views
441

 Published On Jun 19, 2024

Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima ameshauri mamlaka ya kisiasa ya Rais yafungwe ili Rais yeyote atakayekuwa madarakani asitoke nje ya mipango iliyowekwa na nchi ili kuepusha hali ya kila Rais kuwa na vipaumbele vyake.

Askofu Gwajima amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Serikali na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2024/25 ambapo amesisitiza kwamba nchi isipofanya hivyo "kuna siku itaangukia pua."

Aidha, amesisitiza umuhimu wa mipango ya wizara na taasisi mojamoja pamoja na ilani za vyama za uchaguzi kuakisi malengo yaliyomo kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa muda mrefu.

show more

Share/Embed