WASICHANA ISIOLO WAFUZU NA TAALUMA YA USHONAJI NGUO KWA CHEREHANI
Waso TV Waso TV
4.97K subscribers
337 views
3

 Published On Sep 17, 2024

Wasichana ishirini kati ya themanini wafuzu na taaluma ya ushonaji kwa cherehani

Takriban wasichana ishirini hapa isiolo wanakila sababu ya kutabasamu hii ni baada ya kufuzu na kozi ya ushonaji kwa cherehani kisha kukabidhiwa vyeti na cherehani.

Ishirini hao ni Miongoni mwa wasichana themanini ambao walikuwa wakipokea mafunzo ya cherehani kwa kipindi cha miezi mitatu .

kwa mujibu wa sheikh salat Jillo ambaye ni mkurugenzi wa shirika la kikundi cha waislamu cha Al Ansaar amesema kuwa mafunzo hayo yametekelezwa chini ya mradi wa kikundi cha waislamu cha Al Ansaar .

Wengi wa wasichana hao walikuwa wamefuzu darasa la nane na masomo ya shule ya upili na wanatoka familia walio chini kimapato .

Kwa upande wake Bwana Peter Njuguna ambaye ni msaidizi wa kamishna wa gatuzi la isiolo ametoa wito kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na serikali ya gatuzi la isiolo kuungana ili kupiga jeki juhudi za shirika hilo .


Naye Sheikh Hassan Bonaya ambaye ni mwenyekiti wa baraza la wahubiri isiolo amesema mradi huo utawafaidi pakubwa wanufaika hao .

Wakati huo huo bi Ralia wario kutoka Merti amewahimiza wasichana na akina mama kujitokeza kupokea mafunzo ya kushona kwa cherehani ili iwafaidi kiuchumi.

Baada ya Ralia kuzungumza, ismail yasin ambaye ni mzazi amewahimiza wazazi kuwaruhusu mabinti zao wahudhurie masoma ya aina hiyo kwa faida yao .



Join this channel to get access to perks:
   / @wasotv  

WASO TV - Informing and Entertaining

show more

Share/Embed