Angalia Morrison alivyopigana ngumi uwanjani_Nahodha John alivyokosa Penati_Ruvu Shooting Vs Simba
Richard Sosten itatilo Richard Sosten itatilo
630 subscribers
840 views
2

 Published On Oct 26, 2020

SIMBA imekwama tena, Uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam, baada ya kukubali
kichapo cha bao 1-0 na Ruvu Shooting,
inayonolewa na Boniface Mkwasa.
Hii ni mechi ya pili mfululizo, Simba kupigwa
bao 1-0, ilianza na Prisons Oktoba 22 Uwanja
wa Nelson Mandera, Rukwa.
Kipindi cha pili hakikuwa rahisi kwa Simba,
kwani ilijikuta ikitumia nguvu kupambana
kukomboa bao, huku kocha akifanya
mabadiliko kwa wachezaji watatu.
Kocha alimtoa Kahata na kumuingiza Benard
Morrison dakika ya 54, Mzamiru Yassin
nafasi yake ilichukuliwa na Said Ndemla (62)
na dakika ya 70 alimtoa Larry Bwalya,
akaingia John Bocco.

KADI NYEKUNDU

Dakika ya 80 beki wa Ruvu, alimchezea rafu
Miquissone, ambapo mwamuzi Abdallah
Mwinyimkuu aliamuru ipigwe penalti ndipo
vurugu zilianza.
Dakika 82 kiungo wa Ruvu Shaban Msala
alikwenda kumpiga ngumi Morrison,wakiwa
katika harakati za mabishano, jambo lililoibua
mzozo mwingine ambao ulichukua takribani
dakika mbili.
Kiungo huyo alipewa kadi nyekundu
kutokana na tukio hilo,ambapo baada ya
kutokana akawa anajibizana na mashabiki wa
Simba kwa kuonyeshana vidole.
Mpaka sasa Simba imedondosha pointi nane
hadi sasa katika mechi nane, imefungwa
mbili, sare moja na imeshinda tano.

MABEKI wa Ruvu Shooting, wamefanikiwa
kudhibiti kasi za viungo washambuliaji wa
Simba, kupenya ngome yao katika dakika 45
za kipindi cha kwanza.
Winga wa Simba, Ibrahim Ajibu na Francis
Kahata walikutana na mabeki visiki Juma
Nyoso na Renatus Ambros ambao waliitumia
vyema miili yao mikubwa kukaba kwa
kutumia nguvu.

DAKIKA 15 ZA KWANZA

Mechi ilianza kwa kupooza na kufanya
makipa wa timu hizo, kutokuwa na
kashikashi ya kuokoa hatari za
washambuliaji.
Simba ilikuwa inaanzia mashambulizi yake
pembeni, kutokea kwa Shomari Kapombe
(kulia) na Mohammed
Hussein'Tshabalala' (kushoto),ambapo mipira
walikuwa wanawapa Ibrahimu Ajibu na
Francis Kahata.
Dakika ya tisa, Simba ilipata faulo nje ya 18
baada ya beki wa Ruvu Shooting, Renatus
Ambros kumchezea rafu Ajibu ambaye alipiga
mwenye na shuti lake kupita pembeni ya goli.
Kwa upande wa beki ya Ruvu, ilivyokuwa
inaongozwa na Santos Mazengo, Renatus
Ambros, Juma Nyoso na Zuber Dabi,
ikionekana kutumia nguvu na kuzuia njia ya
kupenya washambuliaji wa Simba.
Ukiachana na dakika 15 za mwanzo dakika ya
34 Luis Miquissone alipiga shuti lililolenga
golini, alikosimama kipa Abdallah Rashid,
aliyeudaka mpira kwa umahiri.
Dakika ya 35 Ruvu Shooting, ilipata bao
kupitia kwa Fully Maganga baada ya mabeki
wa Simba kuchanganyana wakiwa katika
harakati ya kuokoa mpira wa hatari.
Baada ya bao hilo ni kama liliwavunja moyo
mashabiki wa Simba, walioonekana wamepoa,
huku wengine wakiona ngumu kupata bao
kutokana na wachezaji waliosimama safu ya
ushambuaji kuonekana wanakosa nafasi
walizopata.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza
zinamalizika Ruvu ilikuwa mbele kwa bao
1-0.

#vuruguuwanjani
#vurugusimbanaruvushooting
#simbavsruvushooting
#golilaleo
#ruvushootingfc
#simbasc
#yangasc
#golilaruvushootingleo
#mechiyaleo
#livesimbavsruvushooting
#magoliyote
#kochawasimba
#simbavsruvushooting
#magaliyaleo
#magoliyaruvushooting
#morrison
#ugomvi
#kochawasimba
#manara
#yangasc
#msimamowaligikuu
#penatiyaleo

show more

Share/Embed