Mvutano wa Kisheria Waanza Kesi ya Boniface Jacob, Andiko Kuhusu Mafwele Lawekwa Kwenye Mashtaka
The Chanzo The Chanzo
80.4K subscribers
721 views
7

 Published On Sep 19, 2024

Boniface Jacob ameweza kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Septemba 19,2024, ambapo Wakili wake Peter Kibatala ameweza kueleza kuwa maamuzi ya dhamana yake yatatolewa mnamo jumatatu ya Septemba 23, 2024.

Hati ya Mashtaka ya kesi inayomkabili Boniface Jacob inaeleza kuwa anatuhumiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, kifungu cha 16.

Katika shitaka la kwanza linaeleza kuwa Boniface Jacob mnamo Septemba 12, 2024, akiwa Dar es Salaam alichapisha taarifa za uongo zikieleza kuwa; "...Mafwele anatuhumiwa na familia nyingi kama mtu ambaye ameshiriki mauaji kwa moja katika kuwapoteza ndugu wa baadhi ya familia zao; kupotea kwa Mfanyabiashara Mussa mziba, Kupotea kwa Deo Mugasa, Kupotea kwa Adinani Hussein Mbezi, Kupotea kwa vijana watano wa Aggrey.." katika mtandao wa X (zamani uliojulikana kama X0 akitumia jinal la Boniface Jacob@ExmayorUbungo akikusudia kuudanganya umma.

Unaweza kutufuatilia kupitia;

TWITTER:   / thechanzo  
INSTAGRAM:   / thechanzo  
FACEBOOK:   / thechanzo  
TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_...
Au tembelea tovuti yetu: https://www.thechanzo.com

Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105

The Chanzo Initiative, 2024 © All Rights Reserved.

show more

Share/Embed