#Highlights_Goli
Richard Sosten itatilo Richard Sosten itatilo
630 subscribers
112 views
3

 Published On Oct 31, 2020

MUSOMA. Akili, nguvu na kasi aliyotumia
winga wa kulia, Ditram Nchimbi na kazi
nzuri aliyoifanya Straika, Michael Sarpong
imeiwezesha Yanga kuibuka na pointi tatu
muhimu katika mchezo wao dhidi ya Biashara
United.
Katika mchezo huo ambao unapigwa Uwanja
wa Kumbukumbu ya Karume mjini hapa,
haikuwa kazi rahisi kwa timu hiyo kuweza
kuondoka na alama tatu kutokana na
ushindani ulivyokuwa kwa wapinzani hao.
Hesabu nzuri na mbinu alizotumia Kocha
Cedrick Kaze kwa mabadiliko alipomtoa
Waziri Junior ambaye alionekana kupoteza
mipira mingi na kumwingiza Tuisila Kisinda,
ilichangamsha mpira na kusababisha matokeo
hayo mazuri.
Ilikuwa dakika ya 76 ambapo Nchimbi
alipotumia akili kufuata mpira uliokuwa
unaelekea nje na kuuondoa kwa pasi nzuri
ambayo ilimkuta Sarpong kwa kichwa na
kuujaza mpira wavuni.
Bao hilo lilionekana kuwachangamsha Yanga
wakiendelea kulisakama lango la wapinzani
na dakika ya 86 Sarpong alikosa bao la wazi
baada ya kupokea pasi fupi ya Yacouba
Songne ndani ya 18 na shuti lake kuishia
mikononi mwa Kipa Daniel Mgore.
Hata hivyo katika mechi hiyo, Makocha wa
timu zote walifanya mabadiliko, ambapo
Yanga iliwatoa Waziri Junior, Ditram Nchimbi
(aliyeumia) na Feisal Salum na kuingia Tuisila
Kisinda, Yacouba Sogne na Zawadi Mauya.

#golilayanga #yangavsbiasharaunitedleo #magoliyaleo #simbasc

show more

Share/Embed