GOOD NEWS: Mtoto wa Ray Alamba Shavu Nono, NMB
Global TV  Online Global TV Online
5.03M subscribers
149,025 views
543

 Published On Feb 24, 2018

GOOD NEWS: Mtoto wa Ray Alamba Shavu Nono, NMB

MTOTO wa Staa wa Filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’, aitwaye Jaden Kigosi, amepata shavu kutoka Benki ya NMB, ambapo amefunguliwa akaunti ya ‘NMB Mtoto Akaunti’ kwa ajili ya akiba itakayoweza kumsaidia hapo baadaye.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumfungulia akaunti hiyo, Makao Makuu ya Benki ya NMB, Posta jijini Dar, Ray alisema kuwa, amefurahishwa na hatua ya benki hiyo kumpokea mwanaye Jaden kufungua akaunti ya NMB Mtoto Akaunti jambo ambalo hata yeye alikuwa akilitamani sana japo hakujua wapi angeweza kumfungulia akaunti kwa ajili ya maisha yake ya badaye.

“Niwaombe tu mastaa wenzangu kuwa, suala la mtoto kumfungulia akaunti benki ni ya muhimu sana kwani sisi wazazi tupo leo lakini hatujui kesho yetu itakuwaje?

“Ili usimnyime haki ya maisha mazuri mwanao hapo baadaye, basi ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anamfungulia akaunti mwanaye ila hata asipokuwepo ataweza kusoma bila shida,” alisema Ray.

Ray aliambatana na mzazi mwenzake ambaye pia ni msaniiwa Bongo Movies, Chuchu Hans katika kumfungulia mtoto wao NMB Mtoto Akaunti.

Kwa upande wake Meneja Huduma za Kibenki NMB, Caroline Mosha, ametoa wito kwa walezi na wazazi kuwa na utamaduni wa kuwafungulia akaunti watoto na vijana wao bila kusahau kuwahimiza kuhusu elimu ya fedha

Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe    / uwazi  

FACEBOOK:   / globalpublis.  . TWITTER:   / globalhabari   Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe    / uwazi1  

kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…    / uwazi1      / uwazi1      / uwazi1   WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK:   / globalpublis.  . TWITTER:   / globalhabari   INSTAGRAM:   / globalpubli  .

show more

Share/Embed