Kujitambua na Kuwatambua Watu Wengine Kiroho - Sehemu ya 3
Pastor James Kalekwa Pastor James Kalekwa
1.12K subscribers
70 views
4

 Published On Premiered Nov 7, 2023

“Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.”
2 Kor 5:16 SUV

Watu ni zaidi ya miili na mwonekano wa nje. Kimsingi, watu halisi ni roho
“BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.”
Mwa 2:7 SUV
na miili ni nyumba tu za watu kukaa iwapo duniani.
“Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni. Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi. Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.” 2 Kor 5:1-‬4 SUV‬‬‬‬‬‬

“Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.” Yohana 14:2 (SUV)
Mfano #1: Tumepewa mtoto mwanamume (a son is given)
“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.”
Isa 9:6 SUV

“For to us a child is born, to us a son is given, and the government will be on his shoulders. And he will be called Wonderful Counselor, Mighty God, Everlasting Father, Prince of Peace.”
Isaiah 9:6 NIV

show more

Share/Embed