SHIRIKA LA BIMA ZANZIBAR LATANGAZA MABADILIKO MAPYA NA MUONEKANO MPYA
KTV TZ ONLINE KTV TZ ONLINE
375K subscribers
857 views
0

 Published On Premiered Jan 14, 2024

Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) limezindua mpango wake mpya wa kubadili muonekano na taswira yake kijamii na kibiashara hatua ambayo inalenga kuakisi ukuaji wa shirika hilo sambamba maboresho ya huduma zake kwa wateja.

Hatua hiyo mkakati inahusisha mfululizo wa mabadiliko chanya yanayohusisha muonekano mpya wa nembo ya shirika hilo, muonekano wa nyaraka rasmi za ofisi, maboresho ya huduma kwa wateja sambamba na mabadiliko ya muonekano wa ofisi za shirika hilo.

Hafla ya uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa ZIC imefanyika leo Zanzibar, ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dkt. Saada Mkuya Salum. Pamoja na Waziri Mkuya pia walikuwepo Naibu Kamishna wa Bima Tanzania, Khadija Issa Said, Balozi wa Bima nchini Wanu Hafidh Ameir (Mb), Mwenyekiti wa Bodi ya ZIC, Ramadhani Mwalimu Khamis, Mkurugenzi Muendeshaji wa ZIC Arafat Haji, wafanyakazi, na wadau mbalimbali wa shirika hilo.


Angalia Video Hii Mwanzo mwisho , Kisha Subscribe ili uendelee Kupata Habari Zote.

Follow Ktv Tz Online
Facebook | KTV TZ ONLINE
INSTAGRAM |@ktv_tz_online

Wasiliana nasi kupitia number
+255 717 619 834



Ktv Tz Online Journalists

cc: Sadia Rashid
cc: Sauti Byego

Camera Department"
Dadi Ali
Omar (OJ)
Nassor Shaibu
Abdallah Juma

Editors:
Juma Maulid
Dadi Ali




Video Zingine:
Angalia hapa - Diamond Platnumz Alivyolisha watoto yatima
- Ali Kiba akiwa Oman

   • ALICHOKIFANYA DIAMOND ZANZIBAR HAITOS...  
   • NI KWELI ALI KIBA AMNUNULIA NYUMBA OM...  

show more

Share/Embed