Salama Na SHUSHO SE6 EP06 FULL SHOW|LUKA 11:9-13 PART 1|SendTip MPESA LIPA NO 5578460
YahStoneTown YahStoneTown
397K subscribers
61,839 views
631

 Published On Feb 21, 2022

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460

Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Kabla ya haya mazungumzo sikua nimewahi kukutana na Mwanadada Christina Shusho, ila habari zake nilikua nazo za kutosha tu. Hodari, Dada, Mama, mcheshi, mwenye sauti ya kumuamsha aliyelala, kumuelewesha asiye fahamu na mwalimu kati ya waalimu wa maisha na muziki.

Ilikua faida kwangu mimi kukutana naye na sikuacha kumuangalia kwa admiration ya hali ya juu, kila likilokua linatoka kinywani mwake lilikua funzo kwa upande wangu bila hata ya kujilazimisha. Ukichukulia yeye si moja ya watu ambao naongea nao mara kwa mara, ki ukweli nilifurahi sana. Mama wa watoto na alikua mke wa mtu ambaye kwenye macho ya watu tunaomuona na kumkubali sana hatuwezi kuelewa au kuamini simulizi za mitihani ambayo ameshawahi kupitia mpaka sasa kuwa yeye ni mmoja kati ya wanamuziki HODARI wa muziki huu wa kumtukuza Mungu na kutufundisha wajibu wetu.

Maisha ni safari ndo kitu sote tunajua, ila safari za wengine huwa na mabasi, au lifti, au punda, au kubebwa. Kila mmoja ana njia yake huku sote tukiwa tunataka ‘kufika mjini’. Je yeye ‘alifikaje? Alikua na usafiri? Alibebwa? Alitembea? Alifikishwa au alizaliwa huko mjini? Simulizi ya maisha yake itakufanya utamani kusikia zaidi na zaidi. Toka siku ya kwanza ya kujitambua kwake na kuolewa akiwa na umri mdogo. Biashara za aina gani alishawahi kufanya? Kipi kilimfanya aingie ndoani mapema? Maisha hayo yalikua vipi? Kuhusu wazazi wake? Na ndoto zake wakati akiwa anakua? Kwenye masuala ya dini aliingiaje? Na je kuhusu uandishi? Kuongoza kanisa? Mapenzi yake kwa Kenya na wa Kenya na wanavyomkubali? Je alishawahi kutamani pengine angekua mtu wa KE tu? Mahusiano yake na viongozi wa Siasa wa Kenya? Mahusiano yake na muziki wa nyumbani? Afya ya akili? Malengo yake endelevu? Khadithi za baadhi ya nyimbo zake ikiwa pamoja na Relax?

Mazungumzo tulivu na mtu makini, kama kawaida yangu na wenzangu tunatumai nawe uta enjoy kama nasi tulivyo enjoy, Rafiki.

Love,
Salama.

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible &...  

Follow:
Twitter:   / yahstonetown  
Instagram:   / yahstonetown  
Facebook:   / yahstonetown  

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

show more

Share/Embed